Islamabad: Ikiwa ni ishara ya kupungua mivutano, India na Pakistan ...
16 Januari 2004Matangazo
zimefungua tena njia yao ya reli baada ya kufungwa kwa miaka miwili. Treni ya mwendo wa haraka, ikiwa na abiria 76, iliondoka mjini Lahore nchini Pakistan kueleke Atari, kilomita kama moja nchini India. Na ikarudi kwa kupitia mpakani, ikiwa na abiri zaidi ya 200 kutoka India, ambao walipokelewa kwa shangwe kubwa. Kuanzishwa tena huduma za reli kumefuatia siku 10 baada ya kufanyika mkutano kati ya waziri mkuu wa India, Atal Behari Vajpayee, na rais wa Pakistan Pervez Musharraf, ambapo walikubaliana kuanzisha tena mazungumzo ya amani mwezi ujao.