1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Pakistan na India zakubali kufungua mpaka wa Kashmir

30 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CENT

India na Pakistan zimekubali kufungua mpaka unaolindwa na majeshi katika jimbo la Kashmir linalogombewa na nchi hizo mbili.Hatua hiyo inachukuliwa kurahisisha kazi za kupeleka misaada kwa wahanga wa tetemeko la ardhi lililoathiri eneo hilo la Asia ya Kusini mapema mwezi huu. Tetemeko hilo la ardhi lililotokea Oktoba 8 limesababisha si chini ya vifo 54,000 nchini Pakistan.Kwa wakati huo huo,katika eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India kiasi ya watu 1,300 wamepoteza maisha yao.Jimbo la Kashmir lililotengwa sehemu mbili limesababisha vita viwili kati ya India na Pakistan.