1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Pakistan na India zaafikiana kufungua mpaka wa Kashmir.

19 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEQH

Hatimaye Pakistan na India zimeafikiana kuwasaidia watu waliokumbwa na kadhia ya tetemeko la ardhi katika eneo la Kashmiri,kwa kuwaruhusu watu kupita katika mpaka wa jimbo hilo lenye mzozo baina ya nchi hizo.

Hatua hiyo inakusudia kuwasaidia maelfu ya watu walionusurika kutokana na tetemeko la ardhi la tarehe 8 mwezi huu,ambao bado wanahitaji misaada.

Zaidi ya hapo,India imeondoa hatua yake ya kuzuia mawasiliano ya simu kueleka Kashmir.

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 15,Wakashmir wa upande wa India wameweza kupiga simu moja kwa moja kwa wenzao walio upande wa Pakistan na kuulizia habari za ndugu na jamaa zao kutokana na tetemeko la ardhi.

Wakati huo huo idadi mpya ya watu waliokufa kutokana na tetemeko hilo la ardhi iliyotolewa na maofisa wa Pakistan,sasa inaonesha ni watu 48,000.