Israel inataka kuwa na udhibiti kamili wa usalama mjini Gaza
17 Desemba 2024Matangazo
Katz alisema hii inamaanisha kwamba hata baada ya kuvunja nguvu za kijeshi za kundi la Hamas, jeshi hilo litaendelea kuwa na uangalizi kamili kwenye Ukanda huo kama ilivyo kwenye Ukingo wa Magharibi. Waziri huyo wa ulinzi amesema hawawezi kukubali aina yoyote ya ugaidi dhidi ya watu wa Israel, huku akisema pia hawatokubali kilichotokea Oktoba 7 kutokea tena.Katika Ukingo wa Magharibi kwa kawaida Israel inafanya uvamizi wa mara kwa mara wa kushtukiza katika miji yake kadhaa iliyo chini ya udhibiti wa Mamlaka ya Palestina.