Israel yashambulia Kaskazini mwa Gaza na kuua watu 20
11 Desemba 2024Ripoti zilizotolewa na maafisa wa afya wa Palestina zinasema mashambulio ya Israel ya usiku wa kuamkia Jumatano yamesababisha vifo vya wapalestina zaidi ya 19, katika eneo la Kaskazini mwa Gaza ambako wanaishi Wapalestina waliopoteza makaazi yao.
Miongoni mwao ni watoto wanne,na wazazi wao katika mji wa Beit Lahiya.
Israel haijasema chochote kuhusu shambulio hilo. Wakati huo huo baraza kuu la Umoja wa Mataifa litapiga kura leo kuamua juu ya azimio linalotoa mwito wa kusitishwa vita mara moja, bila ya masharti katika Ukanda wa Gaza.
Azimio hilo ambalo hata hivyo halina nguvu kisheria, pia linatoa mwito wa kuachiliwa huru bila masharti, mateka wote wanaoshilikiwa na kundi la Hamas, na kufunguliwa njia za kupelekwa msaada wa kibinadamu kwa raia wa Gaza na hasa katika eneo linalozingirwa na Israel la Kaskazini mwa Gaza.