JAKARTA: Serikali haikuwaonya raia kuhusu Tsunami
19 Julai 2006Matangazo
Idadi ya watu waliofariki kutokana na Tsunami katika mwambao wa kisiwa cha Java,kusini mwa Indonesia,imeongezeka kufikia 368.Maafisa wamesema,hadi watu 235 bado hawajulikani walipo, mamia wengine wamejeruhiwa na zaidi ya watu 54,000 wamepoteza maskani zao.Serikali ya Indonesia imekiri kuwa haijawaonya wakaazi wake mapema vya kutosha kuhusu hatari ya Tsunami. Waziri wa utafiti,Kusmayanto Kadiman amesema, dakika 45 kabla ya kisiwa cha Java kukumbwa na mawimbi ya Tsunami,serikali ilionywa,lakini haikutangaza onyo hilo kwa sababu haikutaka kusbabisha khofu kubwa.