Janga la COVID-19 limekuwa na athari mbaya zaidi kwa jamii ya watu wa asili milioni 476 kote ulimwenguni. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kupitia ujumbe wake kwa njia ya video amesema ni muhimu kwa nchi kuandaa rasilimali ili kushughulikia mahitaji ya watu wa asili. Makala Yetu Leo, inawageukia watu wa asili wakati wa janga la virusi vya corona. Ungana na Saleh Mwanamilongo.