Kiongozi wa upinzani Martin Fayulu amefungua kesi katika mahakama ya katiba kuyapinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Desemba 30 mwaka uliopita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kipi kitarajiwe huku mshindi Felix Tshisekedi akijiandaa kuchukua mikoba ya uongozi kutoka kwa rais Joseph Kabila? Jiunge na Josephat Charo katika Maoni mbele ya Meza ya Duara.