Jioni ya Jumatano zinachezwa mechi za mwisho za makundi katika kinyang'anyiro cha ligi ya mabingwa Ulaya, Champions League, ambazo zitamalizika kwa kubainisha timu bora zitakazofuzu kuingia duru ya mtoano. Daniel Gakuba amezungumza na Sekione Kitojo, mwanamichezo mstaafu wa Idhaa ya DW Kiswahili.