Shirika la Afya duniani, WHO, lilizindua sera mpya inayopendekeza matumizi ya bomba la sindano na sindano za kisasa na salama zaidi ili kuzuia maambukizi ya magonjwa. Kwa mujibu wa WHO, zaidi ya watu milioni mbili duniani wameambukizwa magonjwa kama vile homa ya ini na virusi vya Ukimwi kupitia sindano zisizokuwa salama.