Mawaziri wa mazingira kutoka mataifa takribani 50 walikutana wiki hii katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo , kwa ajili ya kikao cha utangulizi wa mkutano wa kilele wa COP27, ambapo mataifa tajiri yaliwekewa shinikizo kuongeza matumizi ili kuzuwia mabadiliko ya tabianchi. Maoni mbele ya meza ya duara inajadili uwezekano wa ajenda ya bara la Afrika katika mabadiliko ya tabia nchi.