1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, ushindi wa Maron una maana gani?

Josephat Charo Nyiro15 Mei 2017

Emmanuel Macron ndiye rais mpya wa Ufaransa baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu Marine Le Pen wa chama cha National cha siasa za mrengo mkali wa kulia, katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili ya tarehe 7 mwezi Mei. Je ushindi wake unaiweka wapi Ufaransa kisiasa kuelekea Umoja wa Ulaya na ulimwengu mzima kwa ujumla?

https://p.dw.com/p/2czCG

Katika kipindi hiki cha Maoni mbele ya Meza ya Duara, Josephat Charo anazungumza na Salim Himid, mkaazi wa mji mkuu wa Ufaransa, wa Paris. Ahmed Rajab, mchambuzi wa masuala ya siasa za kimataifa kutoka  London nchini Uingereza. Abdullah Salim Mzee, mchambuzi wa masuala ya siasa na mkazi wa Potsdam, mji mkuu wa Ujerumani, Berlin. Na profesa Nicholas Boaz katika mji mkuu wa Marekani, Washington.