1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia kituo cha kuongoza vita cha Hamas

14 Desemba 2024

Jeshi la Israel limetoa taarifa yake leo hii inayoeleza kuwa kwa mara nyingine limekishambulia kituo cha kuongoza mapambano ya kijeshi cha Kundi la Hamas, kilichojificha katika maeneo ya shule

https://p.dw.com/p/4o90A
Gazastreifen, Nuseirat |Nach israelischem Angriff
Watu wamebeba majeruhi kufuatia shambulizi la Israeli katika ofisi ya posta ambapo watu walikuwa wamejificha huko Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza Desemba 12, 2024.Picha: Khamis Said/REUTERS

Taarifa hiyo iliongeza kwa kusema wanamgambo walikuwa katika mipango ya kuishambulia Israel na kueleza kuwa kundi hilo lilikuwa limejibanza katika eneo ambalo awali lilifahamika kama "Shule ya Yaffa" mjini Gaza.Hata hivyo madai hayo hayakuweza kuthibitishwa mara moja. Mara kadhaa jeshi la Israel limekuwa likisema Hamas wanajificha katika miundombinu ya kiraia, kama shule, hospitali na kuwatumia Wapalestina kana ngao ya kivita, katika ukiukwaji wa sheria za kimataifa. Na kwa shambulizi hilila sasa hakutoa taarifa ya athari zake. Mzozo wa sasa ulianza baada ya Hamas na vikundi vingine kuvamiwa Israel Oktoba 7, 2023, kuua watu 1,200 na kuchukua mateka 250. Na Israel ilianzisha mashambulizi ya kulipiza kisasai kikubwa ambacho, mamlaka za Palestina wamesema, wameua zaidi ya 44,800 huko Gaza tangu wakati huo.