1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG : Afrika Kusini yapinga shutuma juu ya HIV

20 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDKA

Serikali ya Afrika Kusini hapo jana imejibu vikali shambulio kali la juzi lililotolewa na Stephen Lewis mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya virusi vya HIV na UKIMWI barani Afrika dhidi ya sera za nchi hiyo za virusi vya HIV.

Sibani Mngadi msemaji wa Idara ya Afya amesema wanapinga kwa dharao taarifa iliyotolewa na Stephen Lewis kuhusiana na jinsi serikali ya Afrika Kusini inavyokabiliana na changamoto ya HIV na UKIMWI.

Akizungumza katika mkutano unaofanyika mara mbili kwa mwaka huko Toronto Canada hapo Ijumaa Lewis ameishambulia serikali ya Afrika Kusini na kuishutumu kwa sera zake za virusi vya HIV alizotaja kuwa ni za ukingo wa wendawazimu.

Lewis ameikosoa sana serikali ya Thabo Mbeki kwa kusema kwamba kamwe haitaki kutubu makosa kwa kushindwa kuwapatia maskini madawa muhimu kabisa ya kupambana na virusi vya HIV na kwa kupigia debe madawa ya kienyeji ambayo wanasayansi wametupilia mbali kuwa ni ya uongo.