JOHANNESBURG: Afrika Kusini,Kenya na Uganda zashutumiwa na repoti ya mayatima wa UKIMWI
10 Oktoba 2005Matangazo
Serikali za Kenya,Uganda na Afrika Kusini zimeshindwa kuwasaidia mayatima wa UKIMWI katika eneo lililoathirika zaidi na janga hilo duniani.
Shirika la kutetea Haki za Binadamu la Human Right Watch lenye makao yake mjini New York Marekani limesema katika repoti leo hii kwamba watoto wanaokadiriwa kufikia milioni 43 wenye umri wa kwenda shule hawahudhurii shule katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara wengi wao kutokana na athari za UKIMWI.
Repoti hiyo imesema serikali za nchi hizo zimekuwa zikitowa msaada mdogo kwa juhudi za jumuiya kuwasaidia mayatima na kwamba imeipa kisogo elimu ya watoto walioathirika na UKIMWI.