JOHANNESBURG: Viongozi wa makanisa ya Afrika Kusini wameilaumu vikali ...
22 Desemba 2003Matangazo
serikali yao kwa kuwa inakataa kuilaani hadharani Zimbabwe inapokiuka haki za binaadam, na wakasema msimamo wa serikali unalingana na utawala wa kibaguzi. Viongozi wametoa tangazo wakiisihi serikali mjini Pretoria ijitokeze dhahiri kuulaani ukatili wa serikali ya rais Robert Mugabe. Rais Thabo Mbeki alizuru Harare alhamisi wiki iliopita, na akakutana na Mugabe na wanachama wa chama tawala cha Zimbabwe, na pia Morgan Tsvangirai akiwa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani MDC, katika juhudi ya kushawishi pande mbili hasimu kuzungumza. Mbeki amelaumiwa duniani kwa kuendeleza sera ya diplomasia ya chini kwa chini mkabala wa serikali ya Mugabe.