1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANSBERG: Mswaada wa India juu ya utengenezaji dawa nafuu wazusha taharuki kwa waathiriwa wa ukimwi

24 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFTz

Wanaharakati wa Ukimwi nchini Afrika Kusini wamelezea wasiwasi wao juu ya uamuzi wa bunge la India wa kupitisha mswaada unaozuia utengenezaji wa dawa za kupunguza makali ya ukimwi kwa bei nafuu.

Mashirika yakutoa msaada pia yameukosoa vikali mswaada huo ambao wanasema utawaathiri mamilioni ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi duniani.

Serikali ya India inasema inataka sheria itakayoambatana na masharti ya shirika la biashara duniani. Lakini makundi ya afya yanaonya kwamba ni mataifa mengi yanayoendelea yanayotegemea dawa za rahisi kutoka India.

India ndio taifa linalotengeneza kiwango kikubwa cha dawa za bei rahisi duniani na inasemekana kutengeneza nusu ya dawa zote za ukimwi ulimwenguni kwa bei nafuu.