1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JUBA:LRA yataka Afrika Kusini isuluhishe

17 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDL5

Waasi wa LRA wameiomba Afrika Kusini isuluhishe katika mazungumzo ya kuleta amani baina yao na serikali ya Uganda.

Kamanda wa waasi hao Vincent Otti ameliambia shirika la utangazaji la Uingereza BBC kwamba msuluhishi wa sasa kwenye mazungumzo hayo, makamu wa rais wa Sudan bwana Riek, Machar si muadilifu.

Kamanda huyo pia amesema kwamba Afrika Kusini ina uzoefu juu ya kusuluhisha migogoro.

Mazungumzo ya kuleta amani baina ya waasi hao na serikali ya Uganda yanayofanyika kusini mwa Sudan chini ya usuluhishi wa makamu huyo wa rais bwana Machar yaliahirishwa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya pande mbili hizo kushindwa kuafikiana juu ya hatua ya kusimamisha mapigano.