Juni 26: Miaka 75 ya Umoja wa Mataifa
26 Juni 2020Ilikuwa ni hotuba yenye utata mwingi. Ilikuwa hotuba yenye maneno makali dhidi ya jumuiya ya kimataifa. "Hali ya baadaye ya dunia haitakuwa upande wa utandawazi, badala yake upande wa wazalendo", amesema Donald Trump katika Umoja wa Mataifa mwanzoni mwa Septemba mwaka uliopita. Kiongozi huyo wa Marekani ameiweka hali bora ya nchi yake na wananchi wake katika nafasi ya kwanza kabisa".
Kuhusiana na mradi wa kimataifa kwa ajili ya kuhakikisha usalama duniani, hilo rais wa Marekani hakuuma maneno, katika jukwaa la hadhara kuu ya Umoja wa mataifa mjini New York. Amejipigia debe kwamba kwa mtazamo wake kuna hatua kubwa iliyopigwa,hususan katika utwawala wake nchini Marekani, ikiwa ni ujumbe kwa kundi linalomuunga mkono katika uchaguzi.
Rais Trump bado anasisitiza sera yake ya Marekani kwanza.
Alisisitiza kwa mara nyingine tena kuhusu sera yake ya Marekani kwanza. Masuala anayoyapa umuhimu katika Umoja wa Mataifa ni ya maamrisho. Moja ya mambo hayo aliyaandika katika ukurasa wa twitter Disemba mwaka 2016. Muda mfupi kabla ya kuingia madarakani aliushutumu Umoja wa mataifa kuwa ni klabu ya "watu kukutana, kupiga porojo na kujiburudisha tu." Mwaka mmoja baadaye lakini alisababisha mvutano kuhusiana na kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv na kuupeleka Jerusalem, hatua ambayo hadhara kuu la Umoja wa mataifa ilishatolea maamuzi yake.
Hadi hivi sasa kuna hali ya mparaganyiko wa mahusiano, ambapo Umoja wa mataifa ulifikia makubaliano juu ya mabadiliko ya tabia nchi, alikataa kufanyakazi na mkataba wa Umoja wa mataifa kuhusu wahamiaji, akapunguza mchango wa Marekani katika ujumbe wa kulinda amani na kujitoa kutoka katika shirika la Sayansi na Utamaduni UNESCO pamoja na baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa.
Malalamiko ya mapungufu kwa WHO
Pia Trump alililalamikia shirika la afya ulimwenguni WHO kuwa linamapungufu. Kutokana na utendaji wa shirika hilo kabla ya mzozo wa virusi vya corona kusambaa, alilishambulia mwezi Mei, kwamba halitaki kufanya mageuzi na kwamba ni shirika hilo limekuwa kikaragosi wa China. Ametishia kuvunja uhusiano na shirika hilo. Lengo kuu la Umoja wa mataifa ni pamoja na kufanyakazi kwa pamoja na jamii ya kimataifa. Ili kupatikana amani duniani ni lazima kuachana na hali ya kuthamini utaifa.
Soma zaidi:Ujerumani: Tutaisaidia kifedha WHO
Kwa hiyo basi kulikuwa na haja ya kupatikana utaratibu wa mkataba utakaokuwa na ujumuisho wa jumla duniani, ambao ni Mkataba wa Umoja wa mataifa. Wakati wawakilishi wa mataifa 50 wakitia saini mkataba huo wa kuundwa kwa Umoja wa mataifa tarehe 26, Juni 1945 mjini San Francisco , wawakilishi hao walikuwa wamo katika athari za vita viwili vikuu vya dunia.