1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabila afanya mabadiliko katika baraza la mawaziri.

26 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTO0

Kinshasa. Rais Joseph Kabila wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri , akipunguza mawaziri kwa karibu robo lakini akiacha wizara muhimu bila mabadiliko.

Mabadiliko hayo ambayo yalitarajiwa kwa muda mrefu , yalitangazwa katika televisheni ya taifa jioni jana Jumapili, na kumbakisha waziri mkuu Antoine Gizenga mwenye umri wa miaka 82 ambaye aliwahi kuwa makamu kiongozi , wakati wa utawala wa zamani wa nchi hiyo wa Patrice Lumumba na mpinzani wa muda mrefu. Hayo ni mabadiliko makubwa ya kwanza kufanywa na Kabila katika serikali aliyoiunda mwezi Februari kufuatia uchaguzi mkuu nchini humo.