Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na mwenziye Dennis Sassounguesso wa congo Brazzaville wamehakikisha nia yao ya kurejesha amani na kuboresha uhusiano kati ya DRC na Kongo Brazzaville.
https://p.dw.com/p/CHDF
Matangazo
Rais Joseph Kabila amewataka wanamgambo wote walioko mashariki mwa nchi yake watue chini silaha na ameahidi kurejesha amani na usalama kabla ya mwaka huu kumalizika. Aliyasema hayo wakati waziara yake ya siku mbili mjini Brazzaville.