Kabila atangazwa rasmi mshindi wa uchaguzi Kongo
17 Desemba 2011Matangazo
Majaji wa mahakama hiyo iliyo katika mji mkuu Kinshasa wameyakataa matakwa ya upinzani kuwa matokeo hayo yafutiliwe mbali. Mawakili wa mgombea aliyeibuka wa tatu katika kinyanganyiro hicho cha urais na spika wa zamani Vitalis Kamerhe, waliondoka mahakamani humo wakiueleza uamuzi huo wa mahakama kuwa "kinaya ya haki".
Mahakama hiyo iliamua kuwa Kabila ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 48.95 dhidi ya mpinzani wake mkuu Etienne Tshisekedi aliyepata asilimia 32.33. Wiki iliyopita Tshisekedi aliyakataa matokeo yaliyotangazwa hapo awali na alijitangaza kuwa rais wa taifa hilo, huku akitoa wito wa kuhifadhi utulivu.