Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amemchagua waziri wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Ramazani Shadary kuwa mrithi wake katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 mwezi Desemba mwaka huu; uchaguzi ambao ni wa umuhimu mkubwa kwa mustakhabali wa Congo.