KABUL: Hakuna maendeleo kuhusu mateka wa Korea
29 Julai 2007Matangazo
Maafisa wa Afghanistan wamesema,hakuna maendeleo yaliyopatikana katika majadiliano yake pamoja na wazee wa makundi ya kikabila kuhusu hatima ya mateka 22 wa Korea ya Kusini wanaozuiliwa na wanamgambo wa Taliban.Wateka nyara wametishia kuwauwa mateka hao,ikiwa serikali haitowaachilia huru wafungwa kadhaa wa Kitaliban walio jela. Mateka hao wa Korea ya Kusini walikamatwa zaidi ya juma moja lililopita.Mmoja wao ameshauliwa na wanamgambo.