1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Mateka wa Korea waliosalia waachiliwa

30 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUL

Wanamgambo wa Taliban wamewaachilia mateka wanane wa Korea Kusini leo hii na baadae waliwaachilia wengine watatu waliobakia.

Wanaume wawili na wanawake wawili walikabidhiwa kwa maafisa wa Kamati ya Kimataifa ya Chama cha Msalaba Mwekundu katika barabara ya eneo la Janda katikati ya Afghanistan.

Wafanyakazi wa kujitolea wa Kikiristo wa Korea 12 waliachiliwa huru hapo jana katika jimbo la Ghazni baada ya kushikiliwa kwa wiki sita.Kuachiliwa kwao kunafuatia ahadi ya Korea Kusini kuondowa wanajeshi wake kutoka Afghanistan na kupiga marufuku safari za usoni za makundi ya wamisionari wa Korea nchini Afghanistan.

Wakati huo huo wizara ya ulinzi imedai kwamba wanajeshi wake wamemuuwa kamanda mwandamizi wa Taliban kusini mwa Afghanistan. Wizara hiyo imesema katika taarifa kwamba jeshi la Afghanistan limemuuwa Mullah Brodar katika operesheni ya kijeshi iliofanyika mapema leo asubuhi.