1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Mateka waliosalia wa Korea kuachiliwa leo

30 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUO

Serikali ya Korea Kusini na kiongozi wa kikabila nchini Afghanistan wamesema wanatarajia wanamgambo wa Taliban kuwaachilia mateka wao saba waliobakia wa Korea Kusini leo hii.

Wafanyakazi wa kujitolea wa Kikiristo wa Korea 12 waliachiliwa huru hapo jana katika jimbo la Ghazni baada ya kushikiliwa kwa wiki sita.Kuachiliwa kwoa kunafuatia ahadi ya Korea Kusini kuondowa wanajeshi wake kutoka Afghanistan na kupiga marufuku safari za usoni za makundi ya wamisionari wa Korea nchini Afghanistan.

Wakati huo huo Kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi wa Usalama ISAF kinachoongozwa na Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO kimesema mwanajeshi wake mmoja na mkalimani wake wa Kiafghanistan ameuwawa kusini mwa Afghanistan wakati akiwa kwenye doria.