1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wataliban wakubali kukutana na wajumbe wa Korea

3 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBch

Maafisa nchini Afghanistan wamesema,wanamgambo wa Taliban wanaowazuia mateka raia 21 wa Korea ya Kusini,sasa wapo tayari kufanya mazungumzo ya ana kwa ana pamoja na maafisa wa Korea.Wateka nyara hao wameshawaua Wakorea 2 kutoka jumla ya 23 waliotekwa nyara.Wanamgambo wa Taliban wanaitaka serikali ya Afghanistan iwatoe jela wafungwa wa Taliban na badala yake mateka wa Korea ya Kusini wataachiliwa huru.