1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kadinali Woelki asema ni aibu Ulaya inawatenga wakimbizi

Caro Robi
8 Septemba 2017

Askofu mkuu wa Kanisa Katoliki wa Cologne, Ujerumani Rainer Maria Woelki amelaaani vikali mkataba uliofikiwa kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki kudhibiti mmiminiko wa wakimbizi Ulaya kwa kuutaja wa kinyama.

https://p.dw.com/p/2jbAx
Deutschland Trauerfeier für Germanwings-Opfer im Kölner Dom
Picha: Reuters/O. Berg

 Askofu Mkuu huyo amesema ni aibu kwa Ulaya kuingia katika makubaliano kama hayo ili wao waishi kivyao kwa starehe na kwa ufanisi huku wakifanya mipango ya  kuwaweka wakimbizi katika kile kinachoitwa maeneo tete Afrika na kutathmini iwapo wana  haki ya kupata hifadhi wakiwa katika mazingira magumu na hatari.

Woelki amesema kuusifu mpango unaodhibiti wakimbizi wanaokimbia mateso, unamfanya yeye kama Mkristo kufedheheka na siasa zinazozunguka wahamiaji kwa sasa. 

Mkataba kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki uliofikiwa mwezi mwachi mwaka 2016 unasema kwamba wakimbizi wote wanaokwenda Ulaya kwa kutumia maboti kupitia bahari ya Aegen wanapaswa kurudishwa nchini Uturuki, na kwa hatua hiyo serikali ya mjini Ankara badala yake inapata ufadhili wa kifedha kutoka Umoja huo.

Mwandishi: Caro Robi

Mhariri: Saumu Yusuf