Rais wa Rwanda Paul Kagame alifanya ziara nchini Uganda jumapili ambapo mbali na mambo mengine alihudhuria sherehe za miaka 48 ya kuzaliwa kwa Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa kwanza wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Daniel Gakuba amezungumza na Ali Mutasa, mwandishi wa habari akiwa mjini Kampala, kwanza anamuuliza jinsi waganda wanavyoichukulia ziara hiyo ya Kagame.