Kamisheni mpya ya EU inaanza kazi na mwelekeo mpya
1 Desemba 2024Matangazo
Muistonia Kaja Kallas anakua na wajibu muhimu wa kuongoza safu ya ustawi wa diplomasia ya umoja, huku kambi hiyo ikijipanga kuanza kazi kwa Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump mapema mwakani. Kamisheni ya Umoja wa ya Ulaya ndiyo taasisi pekee iliyopewa mamlaka ya kupendekeza Sheria za Umoja wa Ulaya na kuhakikisha utiifu wa sheria katika mataifa wanachama. Kuanza kwa jukumu la kwanza la von der Leyen kama rais wa kamisheni 2019 kulikwenda sambamba na harakati za ulinzi wa mazingira duniani ambapo ilitoa muongozo wa kukabiliana ulinzi wake katika mataifa ya Umoja wa Ulaya uliofahamika kama "Mpango wa Kijani".