1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Mpango wa kuwakamata viongozi wa LRA huenda ukahujumu juhudi za mazunguzo ya amani

3 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFa9

Tume ya kutetea haki za binadamu nchini Uganda imeonya kwamba mpango wa mahakama kuu ya kimataifa wa kuwakamata viongozi wa kundi la wanamgambo wa LRA huenda ukahujumu mpango wa amani unaotarajiwa kumaliza mzozo wa zaidi ya muongo mmoja.

Mapema mwezi huu mkuu wa uhusiano mwema wa makahama ya kimataifa Christian Palme alisema kibali kitatolewa cha kuruhusu kukamatwa kwa viongozi hao waliongoza kampeini za mauaji ya kinyama dhidi ya raia kaskazini mwa Uganda.

Betty Bigombe waziri wa zamani nchini humo ambaye sasa ni mpatanishi wa serikali katika mazungumzo anafanya juhudi za kuodosha tofauti kati ya waasi hao na serikali ya Kampala ili kujaribu kutoa nafasi ya kufanyika kwa utaratibu wa mazungumzo ya amani.