KAMPALA: Serikali ya Burundi na kundi kuu la waasi huenda wakatia sahihi ...
12 Novemba 2003Matangazo
muwafaka kamili, kufuatia miaka 10 ya kupigana vita, wakati wa mkutano wa viongozi mjini Dar Es Salaam , Tanzania, mwishoni mwa juma hili, - kwa mujibu wa wizara ya kigeni ya Uganda jana. Rais Yoweri Museveni wa Uganda anaongoza chanzo cha kijimbo cha kusimamia utaratibu wa kuleta amani Burundi. Serikali ya Burundi ya rais Domitien Ndayezeye na kundi kuu la waasi FDD, wameshakubali kugawiana madaraka, na pia juu ya usitishaji mapigano. Mkutano mjini DSM mwishoni mwa juma hili utawakutanisha viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda na Afrika Kusini. Kadhalika Mwenyekiti wa Muungano wa Afrika, rais Joachim Chissano wa Msumbiji, anategemewa kuhudhuria mkutano huo.