1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Viongozi 2 na wapiganaji wa LRA wajisalimisha kwa wanajeshi wa serikaii

23 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFB3

Makamanda wawili na wapiganaji 10 wa kundi la waasi nchini Uganda LRA Wamejisalimisha kwa vikosi vya serikali vya kijeshi huko kaskazini mwa Uganda.

Hayo ni kwa mujibu wa jeshi la uganda.

Msemaji wa Jeshi luteni Kiconco Tabaro aliliambia shirika la habari la AFP kwamba makamanda hao wawili wa waasi wa LRA wa cheo cha Luteni walijisalimisha pamoja na wapiganaji wapatao 10 kwa wanajeshi wa serikali waliopo katika maeneo tofauti tofauti wilayani Gulu hapo jana.

Msemaji huyo wa jeshi pia amesema hapo jumamosi wanajeshi waliwauwa waasi watano katika mapambano tofauti katika wilaya za Gulu na Kitgum.

Kundi la waasi wa LRA liliuchukua upande wa Uganda kaskazini tangu mwaka 1988 na kusababisha mzozo wa miaka miwili dhidi ya serikali ya Uganda kutokana na kile wanachokiita kutengwa kiuchumi kwa jimbo hilo.