1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni ya uchaguzi Afrika kusini yamalizika

20 Aprili 2009

Jacob Zuma asema ANC haitobadili katiba

https://p.dw.com/p/HaZD
Rais wa ANC Jacob Zuma akihutubia wafuasi wake.Picha: AP

Kiongozi wa chama cha African National Congress ANC Jacob Zuma amesema kuwa chama chake hakina mpango wa kushikilia mamlaka kwa kubadili katiba.

Zuma alikua akizungumza kwenye mkutano wake wa mwisho kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumatano wiki hii.

Chama cha ANC Kina nafasi nzuri ya kuibuka mshindi kwenye uchaguzi huo lakini hata hivyo kinakabiliwa na ushindani mkali zaidi tangu kiingie madarakari mwaka 1994.

Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake katika mji wa Johannesburgg hapo jana Zuma alisema kuwa chama cha ANC kitapata wingi wa viti bungeni.

Zuma pia alisema kuwa chama chake hakina mpango wa kutumia vibaya madaraka kitakapochukua uongozi.Zuma akaongeza kuwa"Kwa miaka 15 ambayo chama cha ANC kimekuwa madarakani hakijayatumia madaraka hayo kuifanyia katiBa mabadiliko na wala hakina mpango kama huo."

Hii ni baada ya madai kutoka kwa chama cha upinzani cha Democratic Alliance DA pamoja na kutoka kwa F:W de Klerk rais wa mwisho wa utawala wa ubaguzi wa rangi nchini afrika kusini kuwa chama cha ANC kina mpango wa kuifanyia katika mabadiliko.

Akitoa wito wa kuwepo kwa umoja miongoni wa wakaazi wa afrika kusini Zuma alisema ,kuwa chama cha ANC kinafanya juhudi za kukabiliana na mzozo wa kiuchumi ambao kwa sasa unashuhudiwa duniani, na pia kuongeza nafasi za ajira.

Wakibeba bendera huku wakiwa na mavazi yaliyo na rangi ya chama cha ANC wafuasi wa zuma walifurika katika viwanja viwili na kumshangilia mgombea wao.

Nelson Mandela
Rais wa zamani Nelson Mandela alipowasili kwenye mkutano wa hadhara kumuunga mkono Zuma.Picha: AP

Kampeni hiyo ya mwisho ya chama cha ANC ilipewa msukumo kwa kuwepo kwa rais wa zamani wa afrika kusini Nelson Mandela.

Katika ujumbe wake ulinaswa Mandela alesema kuwa usindi wa chama cha ANC utaleta vita dhidi ya umasiki na uongozi bora.Mandela akasema"ANC kina jUkumu la kihisoria la kuongoza taifa letu. kuongoza taifa lenye umoja lisilokuwa na ubaguzi."

Kuwepo kwa mandela kwenye mkutano huo pamoja na mgombea wa urais wa chama cha ANC Jacob Zuma huenda kukakipa chama cha ANc nguvu zaidi hata baada ya wadadisi kusema kuwa huenda chama hicho kikapoteza viti vingi bungeni baaada ya kushutumiwa na jinsi kinavyoshgulikia masuala ya umasikini, uhalifu pamoja na maradhi ya ukimwi.

wakati huo huo vyama vya upinzani kikiwermo cha Democratic Alliance DA pamoja na kile cha Ikatha Freedom Party vilikiwa shutumu maafisa wa chama cha ANC wanaokabiliwa na ufisadi kwenye kampeni zao za mwisho siku ya jumamosi.

waandesha mashtaka walitukpilia mbali mashataka ya ufisadi yaliyokuwa yakimkabili Zuma suala ambalo lililonekana kama kumpa uungwaji mkono Mgombea huyo wa urais wa chama cha ANC

Mwandishi:Jason Nyakundi/RTR

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman