1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KANPUR: Upigaji kura waanza nchini India

7 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBq

Upigaji kura umeanza katika jimbo lililo na wakaazi wengi nchini India la Uttar Pradesh katika uchaguzi wa mikoa. Jimbo hilo la kaskazini lina wakaazi milioni 170 na milioni 16 wamejiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi wa kwanza utakaofanyika katika awamu saba kuanzia mwezi huu hadi mwezi ujao.

Maelfu ya maafisa wa polisi wametumwa kushika doria kuzuia machafuko wakati wa uchaguzi huo. Katika uchaguzi uliopita, machafuko makali yalizuka baina ya wafuasi wa vyama hasimu na wagombea ambao wengi wao hivi sasa wanakabiliwa na mashtaka ya uhalifu.

Maofisa wa uchaguzi wamesema wagombea 839 wanashindania viti katika majimbo 62. Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa tarehe 11 mwezi ujao.