1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela wa Ujerumani ziarani Afrika Kusini

P.Martin6 Oktoba 2007

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani hii leo anakutana na rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela mjini Johannesburg.

https://p.dw.com/p/C784
Kansela Angela Merkel (kushoto) na Rais Thabo Mbeki kabla ya majadiliano yao mjini Pretoria
Kansela Angela Merkel (kushoto) na Rais Thabo Mbeki kabla ya majadiliano yao mjini PretoriaPicha: AP

Baadae Merkel atakwenda Cape Town kutembelea mradi unaohusika na athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika ncha ya bara la Afrika.

Siku ya Ijumaa,Kansela Merkel alikutana na Rais Thabo Mbeki mjini Pretoria.Merkel alisifu juhudi za Afrika Kusini katika kusuluhisha migogoro ya bara Afrika.Akatoa mwito kwa Mbeki kuzidi kumshinikiza rais mwenzake nchini Zimbabwe,Robert Mugabe,kukomesha ukiukaji wa haki za binadamu.

Afrika Kusini ni kituo cha pili cha ziara ya Kansela Merkel barani Afrika.Siku ya Jumapili ataelekea Liberia,kituo cha mwisho cha ziara iliyoanzia Ethiopia.