Rais wa Rwanda Paul Kagame alitoa hotuba usiku wa kumkia leo ambayo kwa sehemu kubwa iligusia japo kwa mafumbo mvutano kati ya nchi yake na taifa jirani la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Pamoja na mambo mengine rais Kagame alimshutumu mwenzake wa Congo Felix Tshisekedi kutumia mzozo unaoendelea mashariki mwa Congo kama kisingizo cha kuchelewesha uchaguzi wa mwaka unaokuja.