1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kavelashvili achaguliwa kuwa rais wa Georgia

14 Desemba 2024

Wabunge wa Georgia wamemchagua mchezaji wa zamani wa soka Mikheil Kavelashvili, kuwa rais wa nchi hiyo kupitia mchakato wa uchaguzi uliokumbwa na utata.

https://p.dw.com/p/4o9W5
Georgien | Parlament wählt Micheil Kavelaschwili zum neuen Präsidenten
Mikheil Kavelashvili akipongezwa baada ya kuchaguliwa kuwa rais mpya wa nchi katika bunge, mjini Tbilisi, Georgia Desemba 14, 2024.Picha: Irakli Gedenidze/REUTERS

Kavelashvili ameshinda baada ya kupata kura 224 kati ya 300 kutoka kwa wajumbe wa jopo maalum la uchaguzi linalomchagua rais, linalodhibitiwa na chama tawala cha Georgian Dream, na ambalo limesusiwa na upinzani. Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Uchaguzi, Giorgi Kalandarishvili, amesema Kavelashvili amechaguliwa kuiongoza Georgia kwa kipindi cha miaka mitano. Rais wa sasa Salome Zurabishvili ameutangaza uchaguzi huo kuwa ''batili'' na amekataa kujiuzulu. Waziri Mkuu wa Georgia, Irakli Kobakhidze amesema kuchaguliwa kwa Kavelashvili, kutatoa mchango mkubwa katika kuimarisha serikali ya Georgia, na uhuru wake, pamoja na kupunguza misimamo mikali na kile kinachojulikana kama migawanyiko.