1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Kaya 5,000 zahamishwa kutoka eneo la maporomoko Uganda

16 Desemba 2024

Serikali ya Uganda imesema itazihamisha zaidi ya kaya 5,000 katika eneo lililokumbwa na maporomoko ya ardhi mashariki mwa nchi hiyo, kutokana na ufa mkubwa uliojitokeza, unaotishia kusababisha maafa mengine.

https://p.dw.com/p/4oC9O
Maporomoko ya ardhi Uganda
Watu 36 walikufa katika wilaya ya Bulambuli, mashariki mwa Uganda kutokana na maporomoko ya ardhiPicha: Nakasiita/AP Photo/picture alliance

Maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa mwishoni mwa mwezi Novemba yalisababisha vifo vya karibu watu 36 katika wilaya ya Bulambuli, huku makumi ya wengine wakihofiwa kufariki baada ya kufunikwa na tope.

Soma pia: Vifo vya maporomoko ya udongo Uganda vyafikia 28

Tangu wakati huo serikali imetahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea janga jingine baada ya ufa mkubwa kuonekana ardhini. Wilaya zinazohusika na agizo hilo ni Bulambuli, Mbale, Sironko, Kapchorwa, Kween, Bukwo na Bududa.

Serikali ya Uganda imetoa muda wa wiki mbili kwa wakaazi kuhama kabla ya mamlaka kuingilia kati na kuwalazimisha kuondoka na kusisitiza kuwa wote watakaohamishwa watapewa msaada wa pesa na makazi mapya.