Timu ya Kenya Harambee Stars leo usiku itapambana na timu ya Tanzania Taifa Stars katika mechi ya kuwania kombe la mataifa Afrika nchini Misri. Timu zote mbili zilishindwa katika mechi zao za kwanza na leo, kila timu ni lazima ipate ushindi ndipo iweze kuwa na matumaini ya kupiga hatua mbele. John Juma amemhoji Sekione Kitojo ambaye ni mwanahabari na pia mchambuzi wa michezo kuhusu mechi hiyo.