Kesi dhidi ya Uli Hoeneß yaanza
10 Machi 2014Tunaanzia kusini mwa Ujerumani katika mji wa Munich ambako kuanzia hii leo macho ya wajerumani yanakodolewa katika ukumbi wa korti inakosilikilizwa kesi ya kukwepa kulipa kodi ya mapato Uli Hoeneß anaetajikana kuwa chanzo cha mafanikio ya timu ya Bayern Munich.Mtu mzito aliyeamua kujichongea mahakamani kwamba alikwepa kwa miaka kadhaa kulipa kodi za mapato.Gazeti la "Neue Osnabrücker linatathmini hatima ya Hoeness na kuandika:"Zahma ya watu wanaokwenda kujichongea mahakamani inapiga humu nchini.Kadhia ya Hoeneß imewagutuwa maelfu ya wenye kukwepa kulipa kodi,waliojitajirisha kwa faida za pesa walizoweka katika nchi mfano wa Uswisi na kwengineko ambako hawatozwi kodi za mapato,bila ya kuripoti katika idara za malipo ya kodi za humu nchini.Yadhihirika kana kwamba sekta ya kichini chini ya fedha imekuwa ikiwasaidia watu kuendeleza uhalifu kwa miongo kadhaa na kufaidika pia.Hakuna namna nyengine ya kuielezea zahma hii kubwa iliyozuka ya watu kwenda kujiochongea mahakamani.Wengi kati ya wanaokwepa kulipa kodi za mapato wanatokea katika ile inayojulikana kama "jamii ya walio juu".Kuanzia leo mwenyekiti wa timu ya Bayern Munich,Uli Hoeneß anafikishwa mahakamani.Huu ni mtihani mkubwa kabisa kuwahi kumsibu bwana huyo aliyejipatia jina na sifa katika ulimwengu wa kandanda na pia wa biashara.Hivi sasa Hoeneß anatapa tapa ,makosa ya kutolipa kodi ya mapato yasije yakamtia jela na pengine kutumikia kifungo pamoja na wale waliouwa na wabakaji.
Jinsi sekta ya fedha inavyojitajirisha
Katika wakati ambapo walimwengu wanasubiri kujua hukumu ya aina gani itatolewa dhidi ya Uli Hoeneß,wengine wanapiga hesabu kuupima mzigo wa madeni-kama vile gazeti la "Landeszeitung" linavyoandika:"Gazeti linazungumzia viwango vya juu vya fedha vinavyopindukia uwezo wa binaadam kukadiria.Inapofikia kiwango cha dala bilioni 100 kwa mfano sote tunasalim amri.Hata sekta ya fedha huzungumzia hapo kuhusu kiwango cha "Madeni yaliyokithiri."Ni sekta hiyo hiyo ya fedha inayoitumbukiza serikali katika janga kama hilo la madeni.Mgogoro wa fedha unapozuka serikali ndiyo inayolazimika kuepusha moto usienee.Sasa lakini mzigo wa madeni ni mkubwa mno kwa namna ambayo baadhi ya nchi zinashindwa hata kukidhi majukumu yao ya kimsingi.Mamilioni ya vijana wanajikuta hawana kazi.Sekta za fedha zinakodowa macho na kutegea.Mbinu zao kuona hali ya ukosefu tamaa ikizidi kuwa kubwa bkufika hadi ya kusababisha malalamiko ya umma inadhihirika kuleta tija.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman