1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kgalema Motlanthe rais mpya wa Afrika Kusini

Kalyango Siraj22 Septemba 2008

Alikuwa makamu rais wa ANC

https://p.dw.com/p/FMiN
Bw Thabo Mbeki ameng'atuka madarakani kama rais wa Afrika Kusini jumapili 21.09.08.Picha: picture-alliance /dpa

Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress ANC kimechagua kiongozi wa muda wa nchi hiyo baada ya rais Thabo Mbeki kutangaza kujiuzulu hiyo Jumapili.

Kgalema Motlanthe aliekuwa makamu rais wa chama tawala ndie anasemekana kuchaguliwa kuchukua hatamu.

Hatua ya sasa inadhihirisha kuendelea kwa mpasuko wa kisiasa kuwahi kukimba chama hicho tangu kung'olewa kwa utawala wa ubaguzi wa rangi.

Afrika ya Kusini sasa ina kiongozi mpya.Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP limemnukuu msemaji wa chama tawala cha ANC,akisema chama kimechagua aliekuwa makamu rais wa ANC Kgalema Motlanthe kama kiongozi wa mda. Hii ina maana kuwa atashikilia nafasi hiyo hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika baada a kipindi cha miezi saba kutoka sasa.

Kuchaguliwa kwa Motlanthe kumefuatia kujihuzulu ka Bw Mbeki hiyo jumapili .

Na hii kumfanya rais Thabo Mbeki kuingia katika daftari za kihistoria nchini humo kwa kuwa kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo tangu kuporomoka kwa utawala wa wazungu kujiuzulu wadhifa wake.

Mbeki ni miongoni mwa vigogo wa na wakongwe wa chama cha ANC ambacho kimemlazimisha kung'atuka.

Katika taarifa ya kujiuzulu alisema yeye amekuwa mwanachama cha ANC kwa miaka 52 na hivyo anaheshimu hatua za kamati tenndaji ya chama hicho iliomtaka kujiuzulu

Chama cha ANC kilimtaka afanye hivyo kabla ya muhula wake kumalizika mwaka ujao.Pia kujiuzulu kwake kumekuja siku nane baada ya jaji kutupilia mbali madai ya rushwa yaliyokuwa yanamkabili kiongozi wa chama hicho Jacob Zuma,akitoa dhana kuwa huenda kulikuwa na mkono mrefu wa siasa katika kesi hiyo.

Lakini katika taarifa ya kujiuzulu kupitia Televisheni Bw Mbeki amekanusha madai ya kuwepo uingiliaji wowote wa kisiasa katika kesi inayomkabili mpinzani wake kisiasa na kiongozi wa chama Jacob Zuma.

Aidha alikuwa amesema kuwa angebaki kama anashikila kiti hicho hadi chama kitakapochagua kiongozi mwingine. Na habari kutoka Afrika Kusini zaeleza kama naibu wa kiongozi wa ANC ndie amechukua wadhifa huo.

Uchaguzi wa makamu rais umemaliza uvumi eti huenda spika wa bunge,Baleka Mbete ndie angechaguliwa.

Bw Zuma alikuwa hawezi kuchaguliwa kwa kuwa alikuwa na kesi zinazo mkalbili ingawa ana nafasi ya wasi ya kuwa kiongozi wa taifa hilo baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Mbeki kabla ya kuwa kiongozi wa nchi hiyo alishikilia wadhifa wa makamu rais kwa kipindi cha miaka mitano.