1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Mashambulio ya waasi wa LRA

14 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFXI

Raia wanane wa Sudan wameuwawa baada ya gari lao kuvamiwa na waasi wa LRA Kusini mwa Sudan.

Kwa mujibu habari za Khartoum abiria hao walikuwa wakisafiri kwa gari la serikali ambapo wapiganaji waasi wa LRA waliwashambulia kwa kuwapiga risasi na kuwauwa.

Inaaminika waasi hao wanafanyia oparesheni zao Kusini mwa Sudan na wamekuwa wakipata silaha kutoka Khartoum katika kulipiza kisasi kutokana na serikali ya Kampala kuunga mkono waasi wa SPLA nchini Sudan.

Tangu mwaka 2002 serikali ya Khartoum imewaruhusu wanajeshi wa Uganda kufanyia oparesheni zao dhidi ya waasi wa LRA walioko sehemu za kusini mwa Sudan mpakani mwa Uganda.

Zaidi ya watu milioni 1 wamelazimika kuhama maskani yao kufuatia vita vya miaka 18 kati ya waasi wa LRA na serikali ya Uganda vilivyosababisha mashambulio ya kinyama dhidi ya raia wa Kaskazini mwa Uganda na Kusini mwa Sudan.