1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kibarua kwa timu za Ujerumani kwenye Champions League

16 Desemba 2019

Droo ya raundi ya timu kumi na sita ya ligi ya vilabu bingwa barani Ulaya imefanyika leo huku Bayern Munich wakipangwa kucheza na Chelsea katika mechi itakayoleta kumbukumbu za mwaka 2012.

https://p.dw.com/p/3UuO1
Champions League Achtelfinale - Auslosung in Nyon
Picha: picture alliance/dpa/Keystone/L. Gillieron

Mwaka huo Chelsea waliwabwaga miamba hao wa Ujerumani kwa mikwaju ya penalti kwenye fainali na kuebuka mabingwa wa Ulaya.

RB Leipzig watacheza na Tottenham Hotspur kisha Borussia Dortmund watavaana na Paris Saint Germain katika mojawapo ya mechi zinazotarajiwa kuwa zenye msisimko mno katika raundi hiyo.

Der FC Bayern München trifft im Champions League Achtelfinale auf den FC Chelsea
Bayern Munich watakuwa na kibarua dhidi ya ChelseaPicha: picture-alliance/SvenSimon/F. Hörmann

Barcelona watapambana na Napoli halafu Liverpool wamepangiwa kucheza na Atletico Madrid huku mechi itakayosubiriwa na wengi ikiwa kati ya Manchester City na Real Madrid halafu Juventus watakuwa wanazipiga na Lyon kisha Atalanta ya Italia icheze na Valencia ya Uhispania.

Mechi hizi zitachezwa kuanzia Februari tarehe kumi na nane huku fainali ikichezwa Mei 30 katika uwanja wa Ataturk huko Istanbul Uturuki.