1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kifungo cha miezi mitano jela kwa muandishi wa habari wa Burundi Aloys Kabura

19 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDAs

Muandishi wa habari wa kituo cha kutawanyia habari nchini Burundi ABP Aloys Kabura, amekatiwa adhabu ya kifungo cha miezi mitano jela na mahakama mmoja ya mjini Ngozi kaskazini mwa Burundi. Aloys Kabura ambae yuko gerezani tangu tarehe 31 Mei mwaka huu, amekatiwa adhabu hiyo kwa tuhuma za kuchochea uasi na kuikashifu serikali kuhusu matamshi yake katika kilabu cha pombe kuhusu tukio la tarehe 17 Aprili mwaka huu la kuzuwiliwa waandishi wa habari kiasi ya 30 katika nyumba ya mbunge Mathias Basabose ambae alikuwa akiuhotubia mkutano wa waandishi wa habari kuhusu ufisadi unaoendelea katika serikali ya Cndd-Fdd

Shirika la mareporta wasiyokuwa na mipaka limelaani kifungo cha muandishi huyo wa habari nchini Burundi Aloys Kabura na kusema kuwa wanayo wasi wasi kuhusu mstakabali wa demokrasia nchini Burundi ambako wanasema idara ya upelelezi imechukuwa jukumu la polisi na idara za sheria. Pia shirika hilo la marepoters wasiyokuwa na mipaka linalaani serikali ya Burundi kwamba haitaki kuwaadhibu wale wanaokwenda kinyume na maadili ya chama.