Kim Jong Il afariki dunia
19 Desemba 2011Matangazo
Kim alikuwa pia akiugua maradhi ya kiharusi tangu mwaka 2008, lakini aliwahi kuonekana katika picha akiwa kwenye ziara za karibuni nchini China na Urusi na nyengine ndani ya nchi yake, ambazo zilikuwa zikitolewa na vyombo vya habari vya serikali. Kiongozi huyo wa Kimomunsti aliyekuwa akijuilikana kwa jina la “Kiongozi Mpenzi” anakumbukwa kwa kupenda kwake sigara, konyagi na vyakula vya kifahari.