1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Chido chaipiga Msumbiji

15 Desemba 2024

Kimbunga Chido kimeipiga Msumbiji mapema leo Jumapili na kusababisha upepo mkali na mvua kubwa, baada ya kukipiga kisiwa cha Mayotte na kusababisha vifo vya watu 11 pamoja na uharibifu.

https://p.dw.com/p/4oAC8
Picha za satelaiti za kimbunga Chido, kilipoipiga Mayotte
Picha inayoonesha kimbunga Chido kilichoipiga Msumbiji, baada ya kuathiri kisiwa cha MayottePicha: CIRA/AFP

Kimbunga hicho cha Chido kilionekana kuongezeka nguvu wakati kilipolipiga eneo la Mfereji wa Msumbiji usiku wa jana, karibu kilomita 40 kaskazini mwa jiji la Pemba, hii ikiwa ni kulingana na idara hali ya hewa.

Shirika la kimataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema lipo kwenye eneo hilo kusaidia watu walioathiriwa na kimbunga hicho, ambacho tayari kimeleta uharibifu.

Limesema majengo mengi ya shule, makazi na vituo vya afya yameharibiwa kabisa ama kwa kiasi fulani, na wanashirikiana na serikali kuhakikishia upatikanaji endelevu wa huduma muhimu.