Kimbunga Kiharibifu Chido chazua mtafaruku kati Mayotte
23 Desemba 2024Matangazo
Wenyeji wanaishutumu serikali ya kuelekeza rasilimali adimu za kisiwa hicho kwa wahamiaji kwa gharama zao. Kisiwa hicho cha Ufaransa kina idadi ya watu 320,000 huku watu 100,000 wakitajwa kuwa wahamiaji na wengi wao wao wakiwa na asili ya visiwa vya Comoro vilivyo karibu kilomita 70 tu kutoka katika kisiwa hicho. Wenyeji wa kisiwa hicho wanaona kwamba mamlaka katika eneo hilo inapaswa kuwazingatia wao zaidi katika kuwapatia msaada wa huduma za kijamii lakini kutokana na uwepo wa wahamiaji kutoka maeneo mengine kunawafanya wao kutopata msaada wanaohitaji hasa katika kipindi hiki kigumu. Kisiwa cha Mayotte kilikubwa na kimbunga Chido ambacho kimegharimu maisha ya watu na kufanya uharibifu mkubwa wa nyumba na miundombinu.