1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Bangui kufungua mpaka na DRC.

25 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWJ

Rais wa jamhuri ya Afrika ya kati Francois Bozize jana amesema kuwa nchi yake itafungua mpaka wake hivi karibuni na jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, uliofungwa tangu mwaka 2002 kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Bozize amesema kuwa atakaporejea mjini Bangui atachukua hatua muhimu kuufungua mpaka huo, alisema hayo baada ya mazungumzo na rais wa DRC Joseph Kabila mjini Kinshasa.