1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Hali inatia wasi wasi DRC.

21 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGy

Hali ya usalama katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, inatia wasi wasi na mageuzi katika jeshi la nchi hiyo yanahitajika haraka , ameeleza afisa wa ngazi ya juu wa umoja wa Ulaya jana.

Roeland Van de Geer, mwakilishi maalum wa umoja wa Ulaya katika eneo la maziwa makuu amesema kuwa umuhimu kwa umoja wa Ulaya ni kusaidia uimarishaji wa sekta za amani na demokrasia katika DRC.

Kwa hiyo amesema umuhimu ni kufanya mageuzi katika sekta ya usalama , polisi, na jeshi.

Hali imekuwa ya wasi wasi tangu Alhamis wiki iliyopita wakati wanajeshi wote ambao bado wanawatumikia viongozi wa waasi, ambao wametumikia wadhifa wa makamu wa rais katika kipindi cha utawala wa mpito, walipoamriwa kwenda katika makambi ya jeshi.

Jean-Pierre Bemba na Azarius Ruberwa, ambao makundi yao ya waasi yalipigana vita hadi mwaka 2003, wanapinga hatua hiyo, wakidai kuwa ulinzi wa maafisa 12 wa polisi waliopewa kutokana na amri ya rais hautoshi.